Afya ni Nini?

Afya ni Nini?

Afya ni hali ya ulinganifu kiakili, kimwili na kiroho. Afya ni matokeo ya chaguzi ndogo ndogo za kila siku katika ulaji, unywaji na mtindo wa maisha kiujumla, hivyo ili tuwe na afya njema mtindo wetu wa maisha wapaswa kuwa ule ufatao kanuni za afya.

Je, kuna mahusiano gani kati ya afya na unene?

Wengi huamini kuwa unene ni dalili ya afya njema,wakati wanaweza kuwa sahihi kwa upande mmoja upande mwingine wanakuwa wanakosea.

Nitajuaje kuwa unene / uzito wangu ni salama kwa afya?

Ipo njia rahisi ya kujua kama uzito (unene / wembamba) wako ni salama au la. Njia hii hujumuisha utafutaji wa uwiano wa uzito (katika kilogramu) na urefu (katika mita) yaani Body Mass Index (BMI) kwa lugha ya Kiingereza.

Nawezaje Kujua BMI Yangu?

Ni rahisi tu, pima uzito wako katika Kilogramu (Kg), pima na urefu wako katika mita(M), chukua uzito wako gawanya urefu wako ukiwa umezidishwa kwa wenyewe (kipeo cha pili cha urefu wako) yaani; uzito (katika kilo)/urefu ×urefu (katika Mita).

BMI Formular

Mfano, Bakari ana kilogram 65 na urefu wake ni mita 1.8 hivyo BMI yake inapatikana hivi

BMI Formular

Ni rahisi namna hiyo, uzito katika kilogram gawanya kwa kipeo cha pili cha urefu wako katika mita. Ukishindwa omba msaada kwa mtaalamu wa afya au waweza kuwasiliana nasi, twaweza kukusaidia kukokotoa BMI yako.

 

Je, ni BMI ipi iliyo salama kwa afya?

Baada ya kupata BMI yako linganisha na ufafanuzi hapa chini

BMI chini ya 18.5 inaonyesha kuwa mhusika ana utapia mlo (marasmus) hivyo ale chakula cha kutosha hususani nafaka zisizokobolewa, protini na matunda na mboga mboga kwa wingi.

BMI kati ya 18.5 na 24.9 inaonesha kuwa mhusika ana uzito (unene / wembamba) salama kwa afya,hivyo aendelee kuishi kwa kufuata kanuni za afya.

BMI kati ya 25 hadi 30 mhusika ana unene uliozidi (overweight) hivyo apunguze vyakula vya mafuta na afanye mazoezi ili kupunguza unene.

BMI ya 30 kuzidi,mhusika ana kitambi (obesity) hivyo apunguze vyakula vya mafuta,afanye mazoezi na program yoyote nzuri ili kupunguza unene.

Je, kuna kanuni ambazo mtu akifuata anaweza kuwa na afya njema?

Ndiyo, utafiti wa Sayansi Tiba unaonyesha kuwa ziko kanuni NANE (8) ambazo ikiwa mtu atazifuata atakuwa afya njema na kuepuka magonjwa maelfu.

Ni kanuni zipi hizo?

Ni hizi hapa kwa lugha ya kingereza:

  1. 1) Nutrition (lishe bora)
  2. 2) Exercise (mazoezi)
  3. 3) Water (maji)
  4. 4) Sunlight (mwanga wa jua)
  5. 5) Temperance (kiasi).
  6. 6) Air(hewa safi)
  7. 7) Rest(pumziko).
  8. 8) Trust in God (imani kwa Mungu).

Kanuni hizi zaweza kufupishwa kama NEWSTART yaani MWANZO MPYA.

Katika makala zinazofuata tutajadili kwa kina kila kanuni tukianza na NUTRITION, yaani Lishe bora.

Mpya kutoka kwetu