Lishe Bora

Lishe Bora

Lishe bora ni moja kati ya kanuni kuu nane za afya njema (yaani, lishe bora, mazoezi ya viungo, maji safi na salama, mwanga wa jua, kiasi, hewa safi, pumziko, imani kwa Mungu). Kiumbe hai yeyote anahitaji chakula ili aweze kuishi. Pamoja na kuwa na uwezo wa kuzuia magonjwa Chakula bora ni dawa ya maradhi kama asemavyo Dr Hippocrates maarufu kama Baba wa ya kisasa "Hebu chakula chako kiwe dawa yako"

Aidha ili chakula kiwe dawa sharti kiandaliwe na kuchaguliwa kwa makini vinginevyo chakula ni sumu kwani tafiti zinaonesha asilimia 35 ya Saratani zote hutokana na ulaji mbaya 1

Katika makala hii tutaangalia makundi ya vyakula na faida zake miilini mwetu, aidha katika makala zijazo tutaangalia makosa yanayope- lekea chakula kuwa sumu badala ya dawa.

MAKUNDI YA VYAKULA

Kuna makundi makuu matano ya vyakula nayo ni;

1. PROTINI

Kazi yake mwilini

Protini hutengeneza seli mpya, hukarabati tishu zilizoharibika, hute- ngeneza vichocheo (hormone), hu- saidia ukuaji wa mwili na akili.

Vyanzo vyake
Protini

Aina zote za nyama, mayai, samaki, maziwa, vyakula jamii ya maharage yaani kunde, mbaazi, maharage, soya, choroko n.k

Mpenzi msomaji protini itokanayo na mimea ni nzuri kiafya ukilinganisha na Ile itokanayo na wanyama hii ni kwa sababu pamoja na matatizo mengine protini ya wanyama huwa na mafuta mabaya ya lehemu.

2. KABOHAIDRETI

Kazi yake mwilini

Huupa mwili nguvu na joto.

Vyanzo vyake
Kabohaidreti

Nafaka kama mahindi, mchele, nyama, ulezi, mihogo, viazi n.k

Utaratibu wa kukoboa nafaka ni mbaya kiafya kwani huondoa viinilishe na makapi lishe ambavyo ni muhimu kwa ajili kuzuia saratani, kusaidia umeng'enyaji na kudhibiti kiwango cha sukari mwilini.

3. MAFUTA

Kazi yake mwilini

Kuupa mwili nguvu, kutengeneza baadhi ya vichocheo, kuupa mwili joto na kusaidia ufyonzaji wa baadhi ya vitamin-A, D, E na K (Fat soluble vitamins )

Vyanzo vyake
Mafuta

Siagi, samli, alizeti, parachichi, ufuta, karanga. Mafuta mazuri ni yale ya mimea kama alizeti, aidha mafuta yatumike kidogo tu maana yakizidi huleta magonjwa ya moyo n.k

4.VITAMINI

Kazi yake mwilini

Kuulinda mwili dhidi ya magonjwa, kusaidia uchukuliwaji wa baadhi ya madini- (Chuma, vitamin C).

Vyanzo vyake
Vitamini

Vitamin hupatikana kwa wingi kwa mbogamboga na matunda. Vitamini hazipendi joto kwani huvunjika kirahisi (unstable ) hivyo matunda yaliwe yakiwa "freshi" mboga za majani zisipikwe kwa muda mrefu.

5. MADINI

Kazi yake mwilini

Madini huimarisha mifupa na meno (madini ya Chokaa), husaidia kupambana na upungufu wa damu (madini chuma).

Vyanzo vyake
Madini

Madini hupatikana kwenye vyakula mbali mbali hasa vitokanavyo na mimea.

Mpendwa msomaji Kula kwa ajili ya afya na si kwa ushabiki, maana yake usile kufuata utamu wa chakula bali dhamiria kula ukikusudia kupata virutubisho fulani katika chakula husika. Pia Hakikisha mlo wako unaokula uwe ni mlo kamili, yaani mlo unaojumuisha vyakula toka makundi yote ya vyakula katika uwiano sahihi.