Alama za Vidole Vya Mungu

Alama za Vidole Vya Mungu

Ulimwengu wetu umejawa na viumbe vya asili vingi sana vyenye mionekano mizuri yenye kuvutia ambavyo tukitazama namna vinavyoishi katika mazingira yake hushangaza sana. Watafiti kwa miaka mingi sasa wameendelea kugundua mambo mengi ya ajabu na ya kushangaza yanayopatikana katika mazingira ya asili yanayotuzunguka. Alama za vidole vya Mungu zi wazi katika kazi yake yote ya Uumbaji.

Mungu wetu aliuumba ulimwengu wetu kwa ustadi mkubwa ajabu, mahesabu na mpangilio wa mkubwa. Watafiti leo wanaendelea kugundua kwamba katika viumbe vya asili ipo mifumo mingi ya kimahesabu inayoonekana katika mpangilio na miundo ya viumbe hivyo.

Kwa mfano, upo mfumo mmoja wa kimahesabu unaoonekana katika viumbe vya asili uliogunduliwa na mwanamahesabu aliyeitwa Learnado Fibonacci. Mwana mahesabu huyu aligundua mlolongo fulani wa namba ambao huelezea mpangilio wa vitu vingi katika asili, kama vile kujipanga kwa majani kwenye miti na maua, miundo ya baadhi ya mayai ya ndege na vitu vingine vingi. Kupitia uvumbuzi alioufanya Fibonacci na uvumbuzi mwingine uliofanywa na wanasayansi wengine baada yake, ni dhahiri kwamba ulimwengu wetu umepangiliwa kiustadi mkubwa na kimahesabu ya Muumbaji wetu, vyote hivi hutushuhudia juu ya uwezo mkuu na hekima kuu ya Mungu wetu aliyeviumba vyote tunavyoviona na vile tusivyoviona.

Ulimwengu wetu na viumbe vya asili haviishii kushuhudia juu ya uweza wa Mungu pekee, lakini pia muhimu zaidi hutushuhudia namna Mungu alivyo, yaani tabia yake.

Tunapotazama namna Mungu anavyohusiana na viumbe vya asili tunagundua mengi sana kuhusu tabia ya Mungu wetu, mfano namna ambavyo anajali viumbe vyake, yeye huyavika maua,

“Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti” Mathayo 6:28,

huwajali ndege wa angani na kuwalinda

“Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu;” Mathayo 10:29

Ingawa ulimwengu wetu umeathiriwa sana na dhambi, bado alama za vidole za Mungu wetu zinaonekana kwa dhahiri katika uumbaji wake, popote tunapogeuka na kutazama alama hizo hutupatia farijiko na kutukumbusha juu ya upendo wa Mungu wetu.

Rafiki Mungu anakupenda sana, zitazame alama za vidole vyake katika viumbe vya asili vyenye kuvutia, soma neno lake leo uelewe zaidi kuhusu Mungu huyu akupendaye.

Mpya kutoka kwetu