Upendo Washinda

Feb 25, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Upendo Washinda

Dhambi imeiharibu sana dunia yetu, haihitaji kwenda mbali ili uone madhara ya dhambi, tazama tu mwili wako mwenyewe, makovu na udhaifu ulionao ni ushuhuda tosha wa madhara ya dhambi, kila tunapogeuka tunashuhudia madhara ya dhambi.

Lakini, mpango wa Mungu katika kuitokomeza dhambi na kukomesha uovu ni wa ajabu na kushangaza sana, Biblia inasema "Mungu ni Upendo." 1 Yohana 4:16. Mungu wetu angeweza kukomesha dhambi na uovu kwa kutumia nguvu zake pekee, angeweza kumfanya kila mtu kuwa mtii kwake kwa shuruti, kama ni nguvu za kufanya hivyo anazo kwani hakuna aliye na nguvu kama yeye. Lakini hapa ndipo palipo na maajabu makuu, YEYE HUTUMIA 'UPENDO' kama wakala wake katika kuondoa dhambi moyoni mwa mwanadamu na kukomesha uovu ulimwenguni.

Ilikuwa ni kwa ajili ya kuonesha upendo wa Mungu, Yesu alikuja kufa duniani na wote wautazamo upendo huo wa ajabu na kuupokea, kwa upendo nao pia huitoa mioyo yao kwake Yesu kama Bwana na Mwokozi wao.

Dini ya Yesu si orodha ya masharti tu yakufuata! Hapana, wampendao Kristo hufanya mapenzi yake kutokana na upendo wao kwake ulioamshwa na kitendo kile cha upendo mkuu alichokifanya Yesu pale msalabani, kwani, 'ni kwa upendo pekee upendo huamshwa',

"Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza." 1 Yoh 4:19

Dini ya kweli ya Kristo hailazimishwi, huinuka toka moyoni kama matokeo ya upendo. Leo watu wengi wamepotoshwa na mwovu Ibilisi, kwani wengi humtumikia Mungu wakisukumwa na woga na hofu wala si upendo, kupitia kwa mafundisho mbalimbali ya dini nyingi za ulimwenguni, watu wengi leo wamepotoshwa kabisa kuhusu namna ya kumwendea Mungu, wengi hudhani kuwa ili Mungu awakubali ni lazima wafanye kitu fulani kumfurahisha au kutuliza hasira yake, kwa kweli wengi leo hawasukumwi na upendo wanapomwendea Mungu, bali hufanya kama wajibu pengine ili kupata mema kutoka kwake!

Hebu sote tumtazame tena Kristo pale msalabani, alifanya yote kwa sababu anatupenda, hatuwezi kununua upendo wake kwa chochote kile, tayari anakupenda, ni wakati wako sasa kufungua moyo wako umpokee naye atajaza moyo wako kwa pendo lake na utakuwa tayari kufanya mapenzi yake ukisukumwa na upendo wako kwake.

Rafiki, Mungu wetu ni wa pekee sana, Upendo wake hatuwezi kuuelezea katika mapana yake ipasavyo, ninaungana na Mtume Yohana kwa kusema

"Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu" 1 Yohana 3:1.

Ni kupitia upendo wake Mungu anafanya kazi ya kutusaidia kuondoa dhambi mioyoni mwetu na kuachana na uovu. Kubali kuupokea upendo wake leo, mkabidhi maisha yako nawe uwe mshindi.