Jitazame Umwone Mungu

Feb 26, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Jitazame Umwone Mungu

Nadharia ya uibukaji hutoa madai kwamba wanadamu ni kama wanyama wengine wa mwituni, isipokuwa tofauti yao ni kuwa na ufahamu mkubwa. Nadharia hii huenda mbali zaidi kusema kwamba viumbe hai, ikiwa ni pamoja na sisi wanadamu ni matokeo ya bahati tu. Kulingana na nadharia hii maisha yetu duniani hayana maana kabisa.

Lakini, hii si kweli, binadamu si kama wanyama wengine wa mwituni tu. Kila mmoja wetu ndani kabisa ya dhamiri yake anatambua kwamba kuna kitu fulani kinachotufanya kuwa wa pekee na kwamba maisha yetu yana makusudi maalum. Biblia inasema,

"tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao" Mhubiri 3:11.

Kila mmoja wetu ndani kabisa moyoni mwake anafahamu kuwa maisha yetu ya thamani fulani na kwamba maisha yetu yanamuelekeo fulani wenye hatima ya milele. Tunatambua kwamba sisi si kama wanyama wengine wa kawaida. Hii ni kutokana na ukweli kwamba tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.

"Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu... Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba." Mwanzo 1:26-27

Shetani siku zote amekuwa akifanya kazi kwa bidii kuwafanya watu wasitambue thamani ya maisha yao. Kupitia nadharia ya uibukaji shetani huwafanya watu waamini kwamba wao ni matokeo ya bahati nasibu tu, eti mlipuko mkubwa wa maada uliotokea mabilioni ya miaka iliyopita, na hivyo huwapendekezea wanadamu kwamba hakuna anayewajali. Wengi leo katika nyakati hizi zenye maendeleo makubwa ya Sayansi na Tekinolojia kwa kuuamini uongo huu wa shetani wamejikuta katika hali mbaya, mawazo mengi na hisia mbaya maadamu kwao huona maisha hayana thamani na hakuna anayewajali.

Lakini rafiki, hakuna ukweli mkubwa zaidi ya huu kuhusu asili ya mwanadamu, tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, japo dhambi imeathiri 'sura' ya Mungu miongoni mwa wanadamu, lipo tumaini la kurejea kikamilifu kwenye mfano wake, yaani wanadamu wenye fikra safi, upendo mkamilifu na hata mwili usioharibika.

Rafiki, wewe ni wa pekee sana, hebu jitazame umwone Mungu, alikuumba kwa mfano wake, japo una makovu ya dhambi, Mungu yupo tayari kukusaidia kurejea katika mfano wake kamili, anakualika leo kwa kuyakabidhi kikamilifu maisha yako kwake naye atakupa nguvu ya kurejea katika mfano wake.