Anguko

Feb 27, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Anguko

Unachotakiwa kufanya ni kutazama karibu nawe, tazama ulimwengu unaokuzunguka na jitazame mwenyewe ili ugundue jambo moja. Na jambo lenyewe ni kwamba, kuna kitu hakipo sawa, shida, maumivu na matatizo ya kila namna ni vidhihirisho kuwa Kuna Jambo fulani lilitokea likasababisha mambo kwenda vibaya hivi. Jambo hili huitwa ‘Anguko’.

Dunia ilipotoka mikononi mwa Mwumbaji maisha yalikuwa shwari kabisa. Wazazi wetu wa kwanza, Adam na Hawa waliishi maisha yenye raha pekee ndani ya bustani ya Eden. Lakini Adam na Hawa walipomwasi Mungu mambo yalianza kubadilika.

Kisa cha ajabu kuhusu namna mwanadamu alivyoanguka dhambini kinapatikana katika sura ya 3 ya kitabu cha Mwanzo. Biblia hueleza kwamba shetani akiwa katika umbo la nyoka aliwadanganya wazazi wetu wa kwanza nao walimwasi Mungu.

Tazama haya mazungumzo baina ya nyoka na Hawa...

"Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. ” Mwanzo 3:1-5.

Kwanza kabisa nyoka (Shetani) anajaribu kumwakilisha Mungu mbele za Mwanamke kama mwenye masharti magumu yenye kubana sana na uhuru mdogo. Mungu alisema

" Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika."Mwanzo 2:17

Mungu aliwapa wazazi wetu wa kwanza uhuru mkubwa wa kula matunda ya miti yote ya bustani isipokuwa mti mmoja tu, tena kwa manufaa yao. Nyoka anapokuja anageuza maneno ya Mungu na kumfanya aonekane kama mwenye masharti magumu na uhuru mdogo sana.

Pia Mungu alisema kama wangalikula matunda ya mti ule hakika wangekufa (Mwanzo 2:17). Lakini nyoka anasema kuwa 'hakika hamtakufa', kwa lugha nyingine nyoka anasema kwamba 'Mungu ni muongo, wala haaminiki, amewaambia mtakatufa lakini kwa kweli hamtokufa'

Na mwisho kabisa katika kilele cha uongo wake nyoka anamwakilisha Mungu kama mbinafsi, mwenye kuwanyima viumbe vyake jambo jema, yaani ni anawanyima nafasi ya kuwa kama Mungu.

Kutokana picha mbaya kumhusu Mungu aliyowasilishiwa mwanamke na yule Nyoka, Biblia inaeleza

"Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala." Mwanzo 3:6

Shetani hata leo rafiki anafanya kazi ya kuwaletea wanadamu mitazamo mibaya kumhusu Mungu. Kupitia mafundisho yaliyopotolewa na falsafa za dunia hii wengi leo wana mitazamo mibaya juu ya Mungu wetu. Lakini rafiki ukweli ni kwamba "Mungu ni upendo" 1 Yohana 4:16. Anakupenda na hujishughulisha sana kwa ajili yako.