Kuvunjika Kwa Mahusiano

Feb 28, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kuvunjika Kwa Mahusiano

Awali kabla ya kuingia kwa dhambi ulimwenguni mwanadamu alikuwa katika mahusiano mazuri baina yake na Muumbaji wake, na baina yao (Adamu na Hawa) wenyewe . Hakukuwa na kutiliana mashaka wala hofu katika uhusiano wao. Kila mmoja aliishi na kujitoa kikamilifu kwa ajili ya mwenzake. Katika Biblia tunasoma kwamba mara baada ya Adam kuona mke wake amekula tunda naye akachukua akala (Mwanzo 3:6).

Kama matokeo ya dhambi upendo na amani waliyokuwa nayo hapo awali vikapotea, wakajisikia hatia ya dhambi, walihofu nini kuhusu mambo yajayo na mioyoni wakiwa utupu wa kiroho. Mwanadamu akaanza kumuogopa Mungu kutokana na dhambi yake, Biblia inatuambia Adamu na mkewe walijificha waliposikia Mungu akipita (Mwanzo 3:8).

"Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone. " Mwanzo 3:8

Hata leo dhambi humfanya mwanadamu amtazame Mungu kama si rafiki tena, dhambi humfanya mwanadamu atafute kujificha toka kwa Mungu. Kupitia kwa anasa za Dunia na dini bandia wanadamu hujificha toka kwa Mungu. Katika Biblia ni wazi kwamba si Mungu anayekwenda mbali na wanadamu bali wanadamu ndio wanaokwenda mbali naye.

Kwa mara ya kwanza pale Edeni dhambi ilipelekea kuvunjika katika mahusiano yaliyokuwepo baina ya Mungu na binadamu. Lakini dhambi haikuishia hapo tu bali pia hata mahusiano baina ya mwanadamu na mwanadamu (Adam na mkewe Hawa) yaliathiriwa. Mwanzo 2:12, 13 inaonesha namna ambavyo mahusiano haya yalivunjika, Adamu akimlaumu Hawa wakati hapo awali alikuwa tayari hata kufa naye kwa kukiuka sheria ya Mungu, na hawa naye akatupia lawama kwa nyoka.

Dhambi ni mbaya sana rafiki yangu, huvunja mahusiano baina yetu na Mungu na matokeo yake hata mahusiano baina yetu wanadamu huvunjika. Jambo jema ni kwamba kwa neema ya Mungu tunaweza kurejesha tena uhusiano ule uliopotea baina yetu na Mungu wetu na baina yetu wenye wanadamu. Alipokuwa hapa duniani, Yesu alitupatia kanuni hii ya kurejesha mahusiano yaliyopotea, alisema jambo la kwanza ni

"Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.” Mathayo 22:37-38

Na kisha

"Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako." Mathayo 22:39

Mahusiano baina yetu binadamu kamwe hayawezi kuwa vizuri kama mahusiano yetu na Mungu ni mabaya, hivyo yatupasa kutafuta kwanza kuwa na mahusiano mazuri na Mungu wetu kisha mahusiano baina yetu wenyewe Mungu atatusaidia kuyaweka vizuri.

Nikukaribishe nawe rafiki mpendwa, Yesu huyu aliyetoa maisha yake kwa ajili yako anataka kuwa na mahusiano binafsi nawe, mpokee leo kwani anakupenda sana.