Ahadi ya Kwanza

March 1, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Ahadi ya Kwanza

Dhambi imeleta maafa makubwa sana duniani, jaribu kutakari huzuni na kilio kilichotoka kwa Adamu na Hawa pale waliposhuhudia kwa mara ya kwanza alama za uharibifu unaoletwa na dhambi. Tafakari namna walipoyatazama majani yakianguka kutoka mitini, maua yakinyauka, hali ya hewa akibadilika mara kwa mara na kwa mara ya kwanza waliposhuhudia kifo kwa mtoto wao Habili. Huzuni yao ilikuwa kubwa sana.

Biblia inatueleza kwamba ardhi ililaaniwa kwa ajili ya mwanadamu, michongoma na miiba ingeota juu ya nchi na chakula kingepatikana kwa kufanya kazi ngumu (Mwanzo 3:17,18,19) hii ikiwa ni sehemu katika kumrejesha mwanadamu atambue ubaya wa dhambi, pale wazazi wetu wa kwanza waliposhuhudia uharibifu uliokuwa ukitokea duniani walitambua uhalisia wa dhambi, waliona umuhimu mkuu wa kuishi sawa na sheria za Mungu. Mungu aliruhusu maumivu yawapate kama sehemu ya mafunzo yao waweze kuona ubaya halisi wa dhambi.

Licha ya kwamba wazazi wetu wa kwanza walimwasi Mungu kwa kwenda kinyume na sheria yake, Mungu bado aliwapenda sana, ingawa aliichukia dhambi yao, upendo wake kwao ulikuwa ni mkuu.

Mara baada ya anguko, Mungu alipokuwa akitoa laana kwa Nyoka Mungu alitoa ahadi kuu ya wokovu na ukombozi wa wanadamu.

"Bwana Mungu akamwambia nyoka... nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino." Mwanzo 3:14-15

Kupitia kwa uzao wa mwanamke nyoka (Shetani) atapondwa kichwa naye Nyoka katika kupondwa kichwa atamponda kisigino mmoja kati ya uzao wa mwanamke.

Huyu aliyeahidiwa kwamba atamponda nyoka kichwa ndoye Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, rafiki yangu. Kupitia kwa kifo chake pale msalabani alitupatia ushindi dhidi ya dhambi, ingawa katika kuleta ushindi huo alijeruhiwa sana na mwovu, alivumilia yote ili kutukomboa wanadamu.

Rafiki katikati ya shida zote za dunia hii lipo tumaini, liletwalo naye Yesu mwokozi wetu aliyemponda kichwa nyoka pale msalabani. Mkabidhi maisha yako Yesu leo hii ili ukamilike katika yeye.