Kuishi Kati Yetu

March 10, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kuishi Kati Yetu

Tangu siku za anguko pale Edeni Dunia imekuwa yenye giza la kiroho kupitia kumuelewa vibaya Mungu. Shetani kwa nguvu zake za udangayifu amekuwa akifanya kazi kwa bidii ili wanadamu wamtazame Mungu vibaya. Wamwome Mungu kama mkali asiyeweza kusamehe, asiye na upendo wala huruma, asiyewajali na wamwone Mungu kuwa ni mbinafsi na mwenye kutafuta maslahi yake mwenyewe pekee.

Ni vipi giza hili lingeondolewa? ni kwa namna gani udanganyifu wa shetani uvunjwe na watu wamtazame Mungu halisi kama alivyo? Mungu mwenyewe aliamua kushuka Duniani kudhihirisha ukweli kumhusu Yeye. Biblia inasema,

"Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. " Yohana 1:14

Yesu Kristo, Mwana wa Mungu tangu awali kabla ya kuumbwa kwa chochote kilichopo duniani na nje ya Dunia alikuwepo pamoja na Mungu (Baba), Biblia humuita "Neno" (Yohana 1:1). Hapa ndipo ilipo siri ya kuu, fumbo la mafumbo yote. Hatuwezi kueleza wala kuelewa kikamilifu ni kwa namna gani, Mungu pamoja na ukuu wa uweza wake akafanyika mwili na kuwa mwanadamu.

Biblia kwamba kabla ya kuumbwa kitu chochote, milele zote zilizopita Mungu amekuwa mwenye furaha katika ushirika wa Nafsi tatu. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu wamekuwa wamoja na wenye furaha daima. Hii ni dhahiri katika Maandiko Matakatifu, mfano katika uvuvio wa Roho Mtakatifu, Sulemani aliandika haya maneno yaliyonenwa Mwana wa Mungu juu ya Mungu Baba,

"Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi; Nikawa furaha yake kila siku; Nikifurahi daima mbele zake; " Mithali 8:30.

Yesu angeweza kudumu upande wa Baba Yake Mbinguni daima, angeweza kudumu katika utukufu wake mbinguni akifurahia huduma ya malaika, angeweza kuwaacha viumbe waliomwasi waangamie na kisha kuumba wengine wema! Lakini Biblia inasema,

"Naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. " Wafili 2:6-8

Ni upendo mkuu namna gani, Mungu kujishusha kiasi cha kuja katika ulimwengu uliochafuliwa na dhambi! upendo huu hauna kifani.

Rafiki, mtazame Yesu Mwokozi wako leo, upendo wake kwako ni mkuu mno, alifanya yote kwa ajili yako, mkabidhi maisha yako leo akamilishe mapenzi yake kwako.