Kilele Mtini

March 11, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kilele Mtini

Yesu, Mwana wa Mungu, alikuja duniani na kuishi pamoja na wanadamu (Yohana 1:14). Kwa kuishi kati yetu (wanadamu), Yesu ametuonyesha wanadamu na malaika kwamba Yeye ndiye 'Neno', kwa matendo ya maisha yake aliyadhihirisha mawazo ya Mungu.

Hakuna lugha iwezayo kuelezea ukuu wa upendo unaoonekana kwa kile Yesu alichokifanya kwa kuacha enzi na utukufu wake mbinguni na kuja kuzaliwa katika sehemu ndogo sana ya uumbaji wake iliyomwasi, sehemu iliyojawa maumivu na mateso. Alizaliwa katika mwili mdhaifu wa kibinadamu, na ajabu zaidi hata alipokuja duniani hakuja kama mfalme, bali alitwaa namna ya utumwa. Mwokozi alizaliwa katika familia maskini na kuishi maisha duni, alishiriki mateso na dhiki zote za wanadamu. Mungu Kwa kuishi kati yetu na kushiriki nasi katika dhiki zetu twatambua wazi kabisa kwamba huguswa na matatizo yetu, anayajua si kwa kutazama pekee na kwa uzoefu wa kuishi kati yetu.

Wanadamu kwa kutenda dhambi tunastahili adhabu ya mauti ya milele (Warumi 6:25 ), lakini kwa pendo lake Mungu, Yesu alizichukua dhambi zetu na kufa ili sisi tupone. Maandiko yanasema,

"Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. " 1 Petro 2:24

Katika msalaba wa Yesu lipo fumbo kubwa sana la upendo ambao hatuwezi kuelewa wala kuelezea ipasavyo, msalaba utakuwa ndiyo tafakari yetu hata katika milele zijazo mbinguni. Hebu jaribu kutafakari, Yeye aliye Mwumbaji wa Mbingu na nchi alikubali kudharauliwa, kutemewa mate, kufanyiwa kejeli na matendo mengi mabaya alifanyiwa yote kwa ajili yako na kwa ajili yangu tupate wokovu.

"Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona" Isaya 53:5

Rafiki, Yesu alikufa pale Msalabani na kama ilivyotabiriwa na manabii, na siku ya tatu alifufuka. Ushindi wetu ulipatikana pale msalabani, tunalo tumaini la uzima wa milele. Nafasi ni yetu kuchagua kuipokea zawadi hii aliyotupa Yesu tuweze kuokolewa toka katika mauti tunayostahili, au kukataa zawadi hii na kupotea milele. Nakupendekezea leo pokea zawadi hii, mkabidhi maisha yako Yesu leo kikamilifu aweze kuyaongoza.