Je Wampenda Yesu?

March 12, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Je Wampenda Yesu?

Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi wetu, alikufa kwa ajili yetu ili kutuondolea adhabu ya mauti ya milele tuliyostahili. Upendo wa Yesu ni mkuu mno hakuna lugha iwezayo kuuelezea, Yeye Aliye mwumbaji, mwenye uwezo usio na kikomo kukubali kufa kwa ajili ya viumbe waliokataa kumtii, ni pendo la ajabu sana!

Wanadamu tulipotenda dhambi, Mwokozi wetu Yesu alikuwa tayari kuutoa uhai wake ili sisi tuwe hai. Sisi hatukumpenda Mungu bali yeye alitupenda sisi hata kumtoa Mwanawe afe Kwa ajili yetu (1 Yohana 4:10). Tuutazamapo upendo wa Mungu kwetu, namna alivyomtoa Mwana wake kufa kwa ajili yetu, mioyo yetu hujazwa kwa upendo huo na kutufanya kuwa tayari kuyakabidhi maisha yetu kwake tusikiapo mwito wake mioyoni mwetu.

"Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza." 1 Yohana 4:19

Wakristo wengi leo wamekuwa wakidai kuwa wanampenda Yesu, lakini kwa kweli si kweli bado hawajampenda Yesu, kwani Yesu Mwenyewe alisema,

"Mkinipenda, mtazishika amri zangu." Yohana 14:15

"Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye... " Yohana 14:21

Wote wanaompenda Yesu watazishika amri zake. Wapo leo wanaosema kwamba amri za Mungu zimepitwa na wakati na wengine husema kwamba kifo cha Yesu kilizifutilia mbali amri za Mungu, hapana hii si kweli, Yesu mwenyewe alisema,

"Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. " Mathayo 5:17

Mtume Yohana aliandika kwa habari ya wasemao wanamjua Mungu na hawazishiki amri zake, alisema,

"Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. " 1 Yohana 2:3-4

Rafiki, ukitaka kujua kama kweli unampenda Yesu, ni rahisi, 'utazishika amri zake' la si vyo maandiko yanasema utakuwa ni "mwongo" kusema kwamba unampenda na bila kuzishika amri zake. Inahuzunisha sana kwetu wanadamu kutokumpenda Yesu kwani alichokifanya kwa ajili yetu ni kikubwa sana, upendo wake kwetu ni mkuu mno, kutokumpenda Yesu ni sawa na kudharau kile alichokifanya kwa ajili yetu.

Hatuzishiki amri za Mungu ili kwamba tumfanye Mungu atupende, la hasha! Yeye tayari alishatupenda na anatupenda sana, kuzishika amri zake ni uthibitisho wa upendo wetu kwake, moyo ulioongoka na uliopokea upendo wa Yesu daima hufurahia kuzishika amri za Mungu.

Rafiki, hebu mtazame Yesu leo pale msalabani, mwombe Mungu akuoneshe ukuu wa upendo wake kwako, na kisha muombe akupatie Roho Mtakatifu akuongoze kuyatenda mapenzi ya Mungu leo!