Kutafuta Kilichopotea

March 2, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kutafuta Kilichopotea

Moja kati ya visa ndani ya Biblia vinavyofunua kwa namna ya kuvutia sana juu ya Upendo wa Mungu na mapenzi yake kwa wanadamu waliopotea kinapatikana katika kitabu cha Mwanzo sura ya tatu. Ukisoma sura hii mstari wa nane, Biblia inaeleza kuhusu Adamu na Hawa kwamba...

"Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone." Mwanzo 3:8

Hii ilikuwa ni mara baada ya kuwa wametenda dhambi kwa kuvunja sheria ya Mungu, walipofumbuliwa macho na walitambua kwamba wapo uchi nao wakajificha.

Sasa hapo ndipo yalipo maajabu, upendo wa Mungu wazi wadhihirika. Ni wazi kwamba hakuna mahali anapoweza kujificha mwanadamu Mungu asimwone.

"Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema Bwana. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema Bwana." Yeremia 23:24

Mungu angeweza kutokea nyuma yao, kisha kuwagusa begani na kuwatisha kwa nguvu, lakini hakufanya hivyo. Angeweza kuingia ndani ya bustani huku akipiga kelele na kutamka maneno makali ya laana na adhabu juu yao, lakini hakufanya hivyo. Angeweza kuwaondoa mara moja katika uso wa nchi kwa kuwaangamiza, lakini hakufanya hivyo. Yeye kwa upendo wake mkuu, alitaka kurejesha mahusiano waliyoyavunja Adamu na Hawa, alihitaji watambue kwamba walikuwa wamekosa na wala yeye hakutaka kuwadhuru. Biblia inaeleza...

"Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? "

Ni picha ya kuvutia namna gani ya Mungu. Hii hudhirisha wazi kabisa, kwamba kweli 'Mungu ni upendo', namna alivyojishughulisha kutafuta kiumbe kilichopotea ni ajabu na kushangaza sana.

Mpendwa, mara nyingi katika maisha yetu, wanadamu huwa tunajificha toka kwa Mungu kwa matendo yetu, twayafamu mapenzi ya Mungu lakini hatuyatendi, lakini yeye hutusihi kwa upendo wake tuje kwake atufanye upya. Hebu mkabidhi maisha yako leo, kubali kuwa mtii kwa sheria yake akuongoze siku zote.