Ishi Maisha

March 4, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Ishi Maisha

Mungu alituumba wanadamu ili wafurahie maisha duniani. Haukuwa mpango wake kutokee mahangaiko haya tuyaonayo leo. Njia pekee ambayo ingemuwezesha mwanadamu kuishi maisha ya furaha milele ilikuwa ni kwa kutii sheria ya Mungu. Sheria ya Mungu ni takatifu ambayo kiini chake ni Upendo, upendo kwa Mungu na upendo wanadamu wenzako.

Shetani tangu zamani, enzi za wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa, amekuwa akiwadanganya wanadamu kwamba wanaweza kupata furaha kamili hata kwa kutokutii sheria ya Mungu, aliwashawishi wazazi wetu wa kwanza kwamba wangekuwa katika hali ya juu zaidi kwa kumwasi Mungu. Hivyo leo watu wengi hudhani kwamba furaha ya kweli yaweza kupatikana hata pasipo kutii sheria ya Mungu, wengi hujitafutia furaha katika anasa za dunia, mali na mambo mengine mengi yaliyo ya kidunia.

Wengi hawafahamu njia pekee ya kuishi maisha yenye furaha kamili, Lakini hebu na wakamwulize, Daudi Mtunga zaburi nini kilikuwa chanzo cha furaha katika maisha yake, naye atawajibu

"Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu." Zaburi 40:8

Kama wasipoamini hebu na kuendelea kudhania kwamba mambo ya dunia hii yaweza leta furaha ya kweli hebu waende kwa mtoto wa Daudi, Sulemani wakamuulize, yeye aliyejaribu kujipatia furaha katika anasa za dunia, kamwe hakuwepo mtu na hata kuwepo mtu aliyezifahamu anasa za dunia hii, kamwe hajawahi kuwepo mtu aliyezijua anasa za Dunia kama Sulemani, yeye ukimuuliza kuhusu mambo ya dunia kama yanaweza kuleta furaha kamili, atakujibu

"Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili... nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kujilisha upepo." Mhubiri 1:2, 17

Je rafiki nawe wakata kuyaishi maisha, yaani kama ambavyo aliyakusudia Mungu, maisha yenye furaha kamili, japo tupo katika ulimwengu ulioathiriwa na dhambi, bado yawezekana kuishi maisha yenye furaha halisi, ya kweli na yenye kudumu, na jawabu linapatikana katika sheria ya Mungu, sheria ya upendo, ile iliyowawezesha wazazi wetu Edeni kuwa na furaha kabla ya Anguko, itakuwezesha nawe pia kuishi maisha yenye furaha leo hii, mali, anasa au chochote dunia itoacho hakiwezi kukupatia furaha halisi, ya kweli na yenye kudumu. Mkaribishe Yesu Kristo leo katika maisha yako akuongoze nawe utakuwa na furaha maishani milele.