Thamani Yako Halisi

March 5, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Thamani Yako Halisi

Ulimwengu una mapendekezo mengi kuhusu thamani ya mtu na maisha yake. Baadhi husema kwamba thamani ya mtu hutokana na wingi wa mali anazomiliki, wengine husema hutokana na chakula alacho, wengine husema ni kulingana na mavazi avaayo, na vitu vingine vingi sana wanadamu huvitumia katika kuelezea thamani ya mtu.

Si lazima mtu atamke kwa mdomo kwamba thamani ya mtu anaipimaje. Matendo yetu, namna tunavyohusiana na watu na namna tunavyojitazama wenyewe huonesha namna tupimavyo thamani ya maisha yako na ya watu wengi. Mfano kwa baadhi, pasipo kuvaa mavazi ya gharama kubwa hawezi kufurahia maisha na huwatazama wasio nazo kama hawana thamani, huyu ameweka thamani yake katika mavazi. Au wengine pasipo kuwa na mali nyingi hawezi kufurahia maisha, huyu ameweka thamani yake katika maisha. Si hivyo tu ipo orodha ya vitu vingi ambavyo wengi hutumia kuthaminisha maisha yao na maisha ya wengine!

Lakini je hii ni kweli? Je ni kweli thamani yetu inapimwa kutoka na vitu flani tulivyo navyo?

Biblia inaeleza ukweli kuhusu thamani halisi ya kila mwanadamu, thamani yetu haipimwi kulingana na vitu vya kupita vya dunia hii. Hakuna kitu cha dunia chenye thamani sawa na ya mwanadamu hata mmoja tu, si pesa, umaarufu wala chochote cha dunia.

Kwanza thamani ya kila mwanadamu inapatikana katika ukweli kwamba yeye ni mtoto wa Mungu na aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Biblia inaeleza wote wanaume na wanawake tuliumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26-27). Mungu kwa upendo wake mkuu alituumba wanadamu kwa mfano wake.

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu...Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. " Mwanzo 1:26,27.

Na pili thamani ya kila mwanadamu inapatikana katika ukweli kwamba Yesu Kristo alikufa kwa ajili yake. Kila mtu bila kujali taifa, kabila, lugha wala tabaka lolote lile Yesu Kristo alikufa kwa ajili yake.

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. " Yohana 3:16

Japo kwa kutenda dhambi wanadamu tulipoteza haki yetu ya kuwa wana wa Mungu, kwa kifo chake Yesu pale msalabani tulifanyika upya kuwa wana wa Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana na Mungu wa vyote.

Bali wote waliompokea [Yesu] aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake" Yohana 1:12

Rafiki jitazame leo katika macho ya Mungu, wewe ni wa thamani sana kwake, si kutokana na vitu ulivyo navyo, acha kupima thamani yako na ya wengine kwa viwango duni vya dunia hii, anza kuwatazama wengine katika macho ya Mungu leo uone thamani yao halisi.