Kwa nini Leo?

March 6, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kwa nini Leo?

Wataalamu wa Sayansi ya seli za neva (neurologists) wamegundua kwamba ubongo wa binadamu ndicho kitu tata kupita vyote vilivyopo katika ulimwengu unaojulikana. Ugunduzi unaonesha kwamba katika ubongo wa binadamu kuna mifumo ya uhusiano ya neva (dendritic connections) zaidi ya 10111 (10^111, yaani kwa lugha nyingine sawa na kusema moja ikifuatiwa na sifuri 111) . Idadi hii ni kubwa zaidi hata ya jumla ya idadi ya atom zote zinazopatikana katika ulimwengu unaojulikana (1081, moja ikifuatiwa na sufuri 81).

Imegundulika kuwa ubongo hufanya kazi kwa namna ya ajabu sana katika kutengeza mazoea hatimaye kupelekea tabia, kila tunapofanya jambo jipya ubongo huwa unatengeneza njia mpya wa mpangilio wa seli za neva (neurone) na kwa kulirudia jambo lile ubongo hufuata njia ile ya mpangilio uliotengenezwa hapo awali na kuuimarisha kadri tulidiavyo jambo hilo na hivyo kufanya kuwa rahisi kulifanya wakati mwingine kwani tayari njia ilishatengenezwa katika mfumo wa mishipa ya fahamu ya ubongo.

Hii ni ajabu sana kwani hututhibitishia kabisa kwamba Mungu wetu aliutengeneza ubongo wa mwanadamu kwa namna ambayo inawezesha kwa urahisi ujengaji wa tabia. Wanadamu tunafanya maamuzi ambayo kwa kuyafanya mazoea hatimaye hupelekea kuwa tabia.

Maamuzi tunayoyanya leo wanadamu huamua tutakuwa kina nani kesho. Upo hivyo ulivyo leo kwa sababu ya mfululizo wa maamuzi uliyoyafanya nyakati zilizopita.

Kupitia maandiko ni wazi kabisa kwamba Mungu yu radhi kumchukua kila mmoja wetu kwenda mbinguni siku Kristo ajapo tena, lakini watakaochukuliwa ni wale pekee ambao kwa tabia zao mbingu itakuwa sehemu yenye furaha kwao, na ndio maana katika wakati huu wa taabu hapa duniani tumepewa kazi ya kujenga tabia zetu. Kupitia maamuzi madogo hata makubwa tunayoyafanya hupelekea kujenga mazoea yanayoleta matokeo ya tabia zetu.

Katika Biblia vipo visa vingi vinavyoongelea umuhimu wa kufanya maamuzi sahihi mapema, yaani kwa nini umefanya maamuzi sasa, kwa nini iwe leo si kesho. Mifano michache ni kama Joshua 24:15,25,29; Zaburi 95:7,8 na 1 Wafalme 18:21,. Mtunga Zaburi alisema maneno haya alipokuwa akiwasihi watu kufanya maamuzi pasipo kuchelewa

"Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu; Kama vile huko Meriba Kama siku ya Masa jangwani." Zaburi 95:7,8.

Wengi wetu katika wakati wa kufanya maamuzi muhimu katika maisha aidha makubwa hama madogo husema nitafanya badae au siku nyingine. Hii ni hatari kubwa kwani mtu utayekuwa kesho si uliye leo. Kuna uwezekano mkubwa kabisa kesho usiwe tayari vile ulivyo tayari leo, si kwa sababu maamuzi yale yanakosa umuhimu, bali kwa sababu mtu uliyekuwa jana ni tofauti na yule uliye leo, kama maneno ya mtunga zaburi alivyosema, ‘moyo huwa mgumu’ kwa kusubiri hadi kesho.

Hivyo rafiki yangu katika maisha haya tunapaswa kujenga tabia zikakazofaa kwa maisha ya milele na Mwokozi wetu mbinguni. Kila siku Mungu wetu hutupatia wito mpya wa kufanya au kuachana na mambo flani ili kutuweza kujenga tabia zetu zifae kuishi naye mbinguni, popote usikiapo wito wake hebu usiseme kesho. Pengine ni tabia au mazoea flani mabaya Mungu anakuita uyaache, au pengine umesikia mwito moyoni mwako, Yesu anakuita utoe maisha yako kwake, umkubali kama mwokozi wa Maisha yako na kujikabidhi kwake aongoze maisha yako, hebu rafiki usiseme kesho, itikia mwito wake leo.