Kutoka Katika Shimo la Dhambi

March 7, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kutoka Katika Shimo la Dhambi

Hapo mwanzo kabla ya dhambi kuingia duniani mwanadamu alikuwa mkamilifu katika mambo yote. Mwenye fikra na nia safi, makusudi matakatifu na alikuwa daima mwenye furaha kuwa katika ushirika na Muumba wake. Lakini Kwa kutenda dhambi mwanadamu alijiingiza utumwani kwa Shetani, hali yake ikabadilika, akawa mwenye fikra, nia na makusudi maovu.

Tangu dhambi iingie duniani hata leo wanadamu kwa asili tuna muelekeo wa mambo maovu na hatuwezi kuupinga uovu kwa nguvu zetu wenyewe, ile furaha ya kuwa katika ushirika na Mungu waliyokuwa nayo Adamu na Hawa kabla ya dhambi haipo tena kwa wanadamu walio wadhambi.

Mara nyingi wanadamu kwa jitihada zetu wenyewe hujaribu kuigeuza mioyo yetu miovu kuwa mema, lakini kamwe hakuna awezaye kufanikiwa katika hili, kwani,

"Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye. " Ayubu 14:4

Mwanadamu mdhambi hawezi kuifurahia sheria ya Mungu, wakati mwanzo kabla ya dhambi, mwanadamu daima alikuwa ni mwenye furaha katika kutii Sheria ya Mungu. Biblia inasema,

"Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. " Warumi 8:7

Ni jambo lisilowezekana kwa sisi wanadamu kutoka katika shimo la dhambi kwa jitihada zetu wenyewe. Mioyo yetu ni miovu na hatuwezi kuibadilisha. Elimu, Ustaarabu, kujitawala nia, kujibidiisha hivi vyote vina sehemu yake katika maisha ya mwanadamu, lakini katika kazi hii ya kubadili moyo havina nguvu. Pengine vyaweza kumfanya mtu aonekane mwema mbele ya watu; lakini kamwe haviwezi kuigeuza asili ya moyo wake. Nguvu ya isiyokuwa ya kibinadamu ni lazima itumike ili kuubadilisha moyo mwovu kuwa mtakatifu. Nguvu hiyo anayo Kristo. Ni Yesu pekee anaweza kuwavuta watu kwa Mungu ili wawe safi.

Rafiki, ni kweli tumezama katika shimo la dhambi na hatuwezi kujitoa wenyewe, Kristo pekee ndiye awezaye kututoa. Elimu, tamaduni wala chochote kilichomo ndani ya dunia hakiwezi kubadili moyo wako. Jikabidhi kwa Kristo leo akuwezeshe utoke katika shimo la dhambi na kuwa kiumbe kipya.