Kiumbe Kipya

March 8, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kiumbe Kipya

Moja kati ya kweli kuu za Biblia ni kwamba wanadamu tumezama katika shimo la dhambi na kwa jitihada zetu wenyewe hatuwezi kujitoa humo. Mioyo yetu ni miovu, imejawa na fikra, nia na makusudi maovu. Ni nguvu ya Kristo pekee ndiyo inayoweza kuibadili mioyo yetu miovu kuwa myema. Mwokozi Yesu alisema,

"Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. " Yohana 3:3.

Kwa asili mioyo yetu ni miovu, hivyo tunahitaji kuzaliwa tena, kwa mara ya pili. Maana yake ni lazima mtu apate moyo mpya, nia mpya na maazimio mapya katika maisha yake. Maandiko yanasema,

"Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. " 1 Wakorintho 2:14

Ni Kristo pekee ndiye awezaye kutoa maisha mapya kwa mtu kuweza kuzaliwa mara ya pili kwani maandiko yanasema,

"Ndani yake [Yesu] ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. " Yohana 1:4.

Kwa wale wote wanaohitaji badiliko kamili katika maisha yao, na kuwa viumbe wapya ni lazima wampokee Kristo na kukaa ndani yake. Mtume Paulo anasema,

"Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. " 2 Wakorintho 5:17.

Ndugu mpendwa, lipo tumaini la kupata moyo mpya, kuzaliwa upya na kuwa kiumbe kipya kupitia Yesu Kristo, Mwokozi wetu. Mkabidhi leo maisha yako naye atakufanya kuwa kiumbe kipya, utashuhudia kuona ya kale yakipita nawe kuwa kiumbe kipya.