Mpango kwa Ajili Yako

March 9, 2018
March
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28
S M T W T F S
1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 31
S M T W T F S
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Mpango kwa Ajili Yako

Moja kati ya sifa za ajabu za Mungu wetu wa Mbinguni ni uwezo wake wa kuona mambo mbele. Yeye huziangalia milele zijazo na kuona nini kipo huko, hakuna chochote kinachotokea pasipo yeye kutambua kabla.

Ni habari njema sana isiyo na kifani kwamba Mungu wetu, yeye Mwenye uwezo wa kuona mambo ya mbele sana pia ni Mungu mwenye upendo mkuu. Maandiko yanasema, "Mungu ni upendo" 1 Yohana 4:8. Hivyo basi kwa kuwa Yeye huyatambua mambo yajayo, huweka mipango yake kwa namna ya ajabu tusivyoweza kujua miaka mingi kabla.

Katika Biblia upo mpango mmoja mkuu wa Mungu unaowekwa wazi katika kurasa za Biblia. Nao ni 'mpango kwa ajili yako'. Mpango wa ukombozi kupitia kwa Yesu Kristo, mwana wa Mungu.

Mpango wa ukombozi wako rafiki ni wa ajabu sana, manabii wa kale waliandika juu ya mpango huu mkuu, kupitia kwa mifano na vielelezo mpango huu ulifuniliwa kwa watu wa Mungu vizazi vingi vilivyopita.

Maandiko Matakatifu yote kwa pamoja humshuhudia Yesu (Yohana 5:39), agano la kale hutabiri juu ya ujio wake Duniani, na jipya kueleza juu ya matukio na matokeo ya maisha yake Duniani. Unabii kumhusu Masihi, Mkombozi wa wanadamu unaopatikana katika agano la kale ni wa kushangaza sana, manabii walitabiri mambo mengi kuhusu yeye, ikiwa ni pamoja na namna ya kuzaliwa kwake, mahali atakapozaliwa, jaribio la kuuwawa angali akiwa mtoto mchanga na mengine mengi. Kwa namna ya ajabu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu alitimiliza yote haya yaliyotabiriwa kumhusu Yeye (Masihi) na ukombozi wetu ulifanikiwa pale msalabani. Nabii Isaya alinena,

"Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. " Isaya 53:4-5

Rafiki, Mungu anakupenda sana, aliandaa mpango wa wokovu wako kwa namna ya ajabu kupitia kumtoa Mwanawe mpendwa Yesu Kristo aliyekufa ili upate kuishi, yeye ndiye, 'aliyejeruhiwa kwa makosa yako'. Ni upendo mkuu huu. Pokea wokovu huu leo kwa kumkabidhi Yesu maisha yako.