Jifunze Neno

jifunze neno la Mungu

Header Ads

KANUNI ZA ULAJI


'Chakula ni dawa', kauli hii maarufu iliyojengeka katika maneno ya Dr. Hippocrates imeshuhudiwa kuwa kweli na maelfu ya watu na hata tafiti nyingi za kisayansi zinaendelea kuthibitisha ukweli kwamba matumizi sahihi ya chakula ni tiba tosha kwa maradhi mengi yanayotusumbua wanadamu. Lakini pia hatuwezi kufumbia macho takwimu na tafiti mbali mbali zinazoonyesha madhara ya kiafya yatokayo na ulaji mbaya. Mfano, Shirika la Afya Duniani (WHO) katika taarifa yake juu ya visababishi vya vifo duniani kwa mwaka 2012 ilionyesha kuwa sababu 8 Kati ya 10 huhusiana na mtindo wa maisha hususani ulaji mbaya1 , pia asilimia 35 ya Saratani zote hutokana na ulaji mbaya 2 . Hivyo maneno "juu ya makaburi mengi ingeandikwa 'amekufa kwa upishi mbaya', 'amekufa kwa kulitumia vibaya tumbo lake" 3 ni sahihi kwa namna ya ajabu

Katika makala hili tutaangalia baadhi ya kanuni njema za kufuata katika ulaji. Kanuni hizo ni kama zifuatazo.
  • Kula mlo kamili, yaani mlo wako uwe na aina zote za virutubishi (protini, wanga, vitamin, madini na mafuta)
  • Mlo mmoja upishane na mwingine kwa masaa 4 hadi 5 ili kupumzisha viungo vya umeng'enyaji. • Kula Milo miwili au mitatu tu kwa siku, mlo wa asubuhi na Mchana ni wa lazima, wa usiku wapaswa kuwa mwepesi (kiasi kidogo )
  • Usinywe maji wakati wa kula, maji huzimua (dilutes) asidi meng'enyi (HCl),hivyo kupunguza ufanisi wa umeng'enyaji, kunywa maji dakika 45 kabla au baada ya chakula.
  • Usile chakula cha baridi, mwili hulazimika kukipasha kabla ya kukimeng'enya, chakula au vinywajji vya moto sana huharibu vimeng'enyi pia huongeza uwezekano wa kupata Saratani.
  • Ikiwa unatumia majani ya chai (ya kiwandani­Chai Bora,Green Label n.k) usinywe pamoja na chakula kwani "Tannin" iliyopo kwenye majani hayo huzuia uchukuliwaji wa madini ya Chuma, Chokaa (Calcium) na Zinc 4 
  • Kula pole pole, ruhusu chakula kichangamane na mate kwani mate yana vimeng'enyi (Salivary amylase) pia hulainisha chakula. 
  • Pumzika kabla ya Kula, tembea baada ya Kula na si kinyume chake.Usile ukiwa umechoka kwani umeng'enyaji huhitaji nguvu, kutembea baada ya Kula husaidia umeng'enyaji kwa kuongeza kiasi cha Oksijeni inayoishia mwilini kwani ndiyo iunguzayo chakula. 
  • Tumia chumvi na sukari kidogo sana. Chumvi iliyozidi yaweza kusababisha Kiharusi (Stroke) na Presha (Hypertension ).Sukari huongeza kalori tupu hivyo tumia kiasi kidogo tu. 
  • Usile usiku sana. Kula masaa 3 hadi 4 kabla ya kwenda kulala hii itawezesha viungo vya umeng'enyaji kupumzika wakati sehemu nyingine za mwili zinapopumzika pia, hii itakuepushia ndoto za ajabu na uchovu wakati uamkapo.
 Mpenzi msomaji ikiwa utafuata kanuni hizo utajiepushia maradhi mengi na "chakula chako kitakuwa dawa yako" kama asemavyo Dr. Hippocrates.
KANUNI ZA ULAJI KANUNI ZA ULAJI Reviewed by David machibya on 12:44 PM Rating: 5

Ad Home

Programs

GUNDUA

Orodha ya masomo 26 yatakayogusa maisha yako kwa namna ya pekee katika kumjua Mungu, maisha yetu na ukweli wa Biblia

Tazama Orodha >>
NENO LA SIKU

masomo yatakuwezesha kila siku kumkaribia Mungu kupitia tafari za Neno la lake takatifu.

Tazama Orodha >>
AFYA

Pata makala mbalimbali za afya zitakazokuelimisha juu ya kanuni mbalimbali za afya na nini ufanye ili uwe mwenye afya njema.

Tazama Orodha >>
Powered by Blogger.