Jifunze Neno

jifunze neno la Mungu

Header Ads

Kipi Kipimo Chako?


"Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana. " Luka 5:18 

 Ni maneno aliyoyasema Petro akiwa ameanguka magotini pa Yesu. Petro alitambua uwepo mtakatifu wa Mungu mahali pale, kupitia muujiza uliofanywa na Yesu mbele yake alitambua kuwa alikuwa amesimama na Mmoja aliye na mamlaka juu ya vitu vyote, alitambua kwamba mbele yake alikuwa amesimama Yeye awezaye kuisoma mioyo kama kurasa za kitabu. Wakati ule Petro aliuona upungufu wake, dhambi zake na unyonge wake mbele ya Yeye ambaye ukamilifu wake hauna kipimo.
Historia takatifu pia inatupatia habari za mtu mmoja aliyeitwa Danieli, ambaye alioneshwa katika maono kwamba Mtu mmoja mwenye mwonekano wa ajabu na sauti yake kama sauti ya umati wa watu alisimama mbele yake. Ndipo Danieli anasema maneno haya:

"Nami, Danieli, nikaona maono haya peke yangu...wala hazikubaki nguvu ndani yangu; maana uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikusaziwa nguvu" Danieli 10:8

Hapa tunapewa habari za mtu mkubwa huyu wa Mungu! Danieli, ni yule aliyesimama mbele za mfalme wa Babeli na kumweleza ndoto aliyoiota, ni yule yule aliyetupwa kwenye tundu la simba nao simba hawakumfanya kitu, ni yule yule aliye tafsiri fumbo gumu la mfalme Belshaza. Lakini! mbele zake Mtakatifu (yaani, Yesu) aliyemtokea katika njozi , Danieli anatueleza kuwa "uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu". Licha ya kwamba mtu wa Mungu Danieli alikuwa mnyofu katika njia zake na mwenye kumcha Mungu lakini bado kama mwanadamu wa kawaida, udhaifu wake na dhambi vililetwa katika ulinganifu na ukamilifu wake Mungu na akajiona mpungufu na mchafu.
Vivyo hivyo na kwa wote walioweza kuona taswira ya ukuu na utakatifu wa Mungu.

Nabii Isaya alipouona utakatifu wa Mungu alisema,
"Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi." Isaya 6:5

Petro, Danieli, Isaya na wengine kutoka katika Maandiko walipouona utakatifu na ukuu wa Bwana walitambua udhaifu na unyonge wao. Vivyo hivyo kwetu leo tutaweza kuutambua udhaifu na unyonge wetu pale tutakapomtazama Mwokozi na kuona utakatifu na ukamilifu wake. Mara nyingi hatutambui udhaifu wetu, unyonge na ubaya wa dhambi zetu kwa sababu bado hatujamtazama Mwokozi wetu Yesu katika utakatifu wake. Kwa sehemu kubwa mambo duni ya dunia hii yametupofusha macho kiasi kwamba hatuoni haja ya kutafuta kumwona Mungu katika utakatifu wake. Inasikitisha sana wengi leo hata miongoni mwa wale walitajao na kulikiri jina la Yesu wameruhusu bongo zao kujazwa na vitu duni vya duniani kiasi kwamba tafakari takatifu za mwokozi wao hazipati nafasi katika akili. Badala ya kumtazama Kristo kama kielelezo cha maisha na kipimo cha ukamilifu wengi leo huutazama ulimwengu na mambo ya ulimwenguni. Si ajabu kuona kwamba kuna viburi, kujitukuza nafsi, majivuno miongoni mwa wale wanaomwamini Yesu kwani bado Kristo hajafanywa kuwa tafakari kuu ya bongo zao.

Rafiki, kipi kipimo chako leo? Je wamtazama Kristo katika utakatifu na ukamilifu wa tabia yake? Ni nini kiijazacho akili yako leo, je mambo duni ya dunia hii, au ni tafakari takatifu za Mwokozi wako.  Yatupasa kuzizoesha fikara zetu daima kutafakari juu yake Mwokozi wetu, kuchunguza kwa makini maisha yake alioyoishi na kulinganisha na vile tuishivyo, kwa namna hiyo tutaweza kuutambua upungufu na udhaifu wetu.
Kipi Kipimo Chako? Kipi Kipimo Chako? Reviewed by David machibya on 11:49 PM Rating: 5

Ad Home

Programs

GUNDUA

Orodha ya masomo 26 yatakayogusa maisha yako kwa namna ya pekee katika kumjua Mungu, maisha yetu na ukweli wa Biblia

Tazama Orodha >>
NENO LA SIKU

masomo yatakuwezesha kila siku kumkaribia Mungu kupitia tafari za Neno la lake takatifu.

Tazama Orodha >>
AFYA

Pata makala mbalimbali za afya zitakazokuelimisha juu ya kanuni mbalimbali za afya na nini ufanye ili uwe mwenye afya njema.

Tazama Orodha >>
Powered by Blogger.